Psalms 15

Kitu Mungu Anachotaka

Zaburi ya Daudi.

1 a Bwana, ni nani awezaye kukaa
katika Hekalu lako?
Nani awezaye kuishi
katika mlima wako mtakatifu?

2 bNi yule aendaye pasipo mawaa,
atendaye yaliyo haki,
asemaye kweli toka moyoni mwake,
3 cna hana masingizio ulimini mwake,
asiyemtenda jirani yake vibaya,
na asiyemsingizia mwenzake,
4 dambaye humdharau mtu mbaya,
lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana,
yule atunzaye kiapo chake
hata kama anaumia.
5 eYeye akopeshaye fedha yake bila riba,
na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.

Mtu afanyaye haya
kamwe hatatikisika.
Copyright information for SwhNEN